ZITTO ZUBERI KABWE IS WRONG!

Na, <bongotz.com>

Itakumbukwa kuwa Zitto Zuberi Kabwe (MB) aliposimamishwa ubunge mwaka 2007 kuhusu kile alichokisema bungeni kuhusiana na suala la Buzagwi, tovuti hii iliandika makara ndefu ikisifia hatua yake a kishujaa ya kuweka maslahi ya taifa mbele kuliko yake binafsi. Lakini hivi karibuni mienendo ya mbuge huyu kijana toka jimbo la Kigoma-kaskazini (Chadema) imetufanya tujiulize maswali mengi yasiyo na majibu: Nini kimemkumba Zitto? Je, ilikuwa ni nguvu ya soda tu (Mrema style) au...? Who is the real Zitto?

Hivi karibuni kulizuka mjadala kwenye forum ya Wanabidii kuhusu hoja ya kutenganisha uchaguzi wa urais na wabunge. Maada ambayo ilichangiwa na watu wengi akiwemo Zitto mwenyewe, mhariri wa gazeti la Tanzania Daima (Absalom Kibanda), Managing Editor, The Gurdian on suday (Richard Mgamba); na Excecutive Editor, Tanzania Media Women's Association (TAMWA)-- Ananilea Nkya.

Katika kuchangia mada hiyo, Zitto alikurupuka (a rookie mistake), na kutoa mifano mbalimbali ikiwemo Rwanda ambapo rais anakaa madarakani miaka 7 na wabunge miaka 5. Akaenda mbali kidogo na kutoa mifano ya nchi za dunia ya kwanza kama vile marekani ambapo rais anakaa madarakani miaka 4, maseneta miaka 6, na members of congress (wabunge) miaka 2. Kwenye hitimisho la mjadala, Zitto akesema (kwa ki-inglish), nami namnukuu, " I would go for 6 years Urais and 4 years Ubunge.

Siku iliyofuata, gazeti la Tanzania Daima likaandika habari kulingano na alichokisema Zitto kichwa cha habari kikisomeka, "Zitto: JK aongezewe Muda".

Baada ya hapo, Zitto na wafuasi wake (Wanabidii); Richard Mgamba, pamoja na Ananilea Nkya wakaanza kumshambulia mhariri wa Tanzania Daima ndugu Absalom Kibanda huku wakidai gazeti lake (Tanzania Daima) limuombe radhi Zitto. Kwa ushujaa wa pekee, ndugu Kibanda akajbu na kusema, [hell no!]--"hatutarajii kufanya hivyo!"

Kama Mwanabidii and Chief Excutive Officer wa BongoTz group, sikuona kama ni vema nikae kimya. Hivyo nikaingia na kutoa maoni yangu. Nikaandika na kusema, "Binafsi naona kama wanabidii mmekurupuka kwa hisia za ghafla na kuanza kumshambulia ndugu Kibanda wa Tanzania Daima bila hata kukaa chini na kujiuliza swali la msingi: Kwamba, kwanini Zitto anajaribu ku-push uchaguzi wa Rais uwe miaka 6 na wabunge miaka 4? Yes, baada ya miaka sita (2016) Zitto atakuwa na miaka 40--moja ya sifa anazopaswa kuwanazo mgombea yoyote wa urais nchini. Can't you guys see that he [Zitto himself] created this whole conspiracy storm? Kibanda hakukosea kabisa ku-point out hii conspiracy! And I think wanabidii mnakosea katika hili... Binafsi sioni haja ya kuiga nchi za dunia ya kwanza (Ufaransa na Marekani) ambazo huendesha chaguzi zao za urais/bunge katika vipindi tofauti. Bear in mind kwamba nchi yetu ni masikini sana na uchaguzi una gharama zake. Nchi nyigi za dunia ya kwanza zina kiburi cha kuendesha chaguzi zao kwa nyakati tofauti kwasababu resources za kufanya hivyo zipo. Plus, nchi yetu bado haijabobea hata kidogo katika teknolojia ya kisasa ukilinganisha na nchi ambazo Zitto amezitaja kama mfano wa kuigwa kwenye piece[makala] yake. Chukulia kwa mfano Marekani. Wamarrkani most of the time wanatumia "Electronic Voting Machines" ambazo zinafanya zoezi zima la uchaguzi liwe rahisi/effeciency of voting & results declaration...and also it is cost-effective, too. Kama kweli Zitto ana pure intention ya kutaka kurekebisha mfumo wetu wa uchaguzi, kwanini asipendekeze miaka 4 kwa urais na miaka 6 kwa wabunge. Why 6 yrs for presidency? The answer is simple, he'll be 40 by 2016. Oh, well maybe I am a conspiracist, too... But, my name is Gustanza, The Great and I love my country!" Mwisho wa kunukuu nilichoandika.

Baada ya hapo watu wengi wakakasirika na kutaka mjadala huu ufungwe kwasababu eti sisi tulio wachache hatukukubaliana na matakwa ya walio wengi (wafuasi wa Zitto).

Labda nimnukuu Mwanabidii, Jovias Mwesiga, aliyechangia hoja hiyo pia na kuweka hoja zetu (tulio wachache/tuliopinga hoja ya Zitto) katika maneno matamu yafuatayo, "...kwa demokrasia iliyopana si dhambi mtu kutofautiana na mawazo na uongozi wake kimawazo ilimradi havunji taratibu za chama chake...Tumezoea sana mambo ya kiimra imra ndo maana hata kwenye CCM ikitokea mtu akaongelea vitu vinavyogusa interest za nchi huku serikali ikiwa imeboronga utasikia huyu si mwenzetu mara huyu ana nia mbaya. Nani kakuambia mtu ukiwa kiongozi wa ngazi za juu wa chama ni mtakatifu na [eti] unaloliamini wewe ni sahihi? ...Colin Powel alimsupport Obama sijasikia nyumba yake kitiwa moto wala kufukuzwa Republican sasa ngoja Zitto akutane na Chiligati bar wanunuliane bia mbili tatu kesho utasikia anataka kuhamia CCM. Lazima tufikie mahala tukomae kifikra."

Yes, Wanabidii inabidi mfike mahara mkomae kifikra. Msikurupuke kutetea hoja zisizo na kichwa wala miguuu eti tu kwasababu kasema Zitto. Acheni kuongozwa na hisia. Rather, use facts and evidence to support your arguments/claims.

Mungu ibariki Tanzania!

Tuma maoni [Hapa>]

<<BACK TO MAIN PAGE >>

©Copyright:BongoTz.Com -MMV. All Rights Reserved.