KIKWETE USITANIE VIJANA:HII NDIO KASI MPYA...!?

Na, Edward chacha

Hivi karibuni Bwana Jakaya Mrisho Kikwete--rais wa nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitangaza Bazara lake la Mawaziri ambapo ameunda wizara kadhaa mpya hivyo kusababisha balaza hilo jipya kuwa na wizara nyingi zaidi kuliko ilivyokuwa katika serikali ya awamu ya tatu. Ingawa ametimiza ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni kwa kuwachagua wanawake wengi kwenye baraza lake la mawaziri, ukubwa wa baraza hilo pamoja na kuwarudisha madarakani wazee vikongwe kama Mzee Kingunge Ngombale Mwiru ni dharau kubwa kwa vijana wengi waliokuwa na mategemeo ya kuona mabadiliko ya kweli ndani ya serikali ya awamu ya nne.

Ingawa Bw. Lyatonga Mrema anajulikana kwa kuwa mchemkaji mkubwa, lakini hoja anayoijenga kuhusu ukubwa wa serikali ya awamu ya nne ni ya muhimu na maana kabisa. Wizara zimekuwa nyingi mno, hali inayoashiria matumizi makubwa ya Serikali katika siku za usoni.

Mathalani, dhana ya kutenga jeshi la polisi toka kwenye Wizara ya Mambo ya Ndani na kuunda wizara mpya ya Usalama wa raia ili kuwahakikishia wananchi usalama wao ni uchemkaji usio na maana kabisa! "a big joke!," wazungu husema.

Suluhisho hapa halikuwa kuanzisha wizara mpya, bali suluhisho halisi ilikuwa ni kuhakikisha kuwa uwajibikaji wa kweli unaonekana ndani ya jeshi hilo la unyang'anyi (polisi) ambalo mara kadhaa limekuwa likijihusisha na vitendo viovu kama vile ujambazi pamoja na rushwa. Uwajibikaji gani?--Fukuza kazi mkuu wa jeshi hilo kama ameshindwa kazi ya kuhakikisha kuwa jeshi lake linafuata miiko ya kazi. Fukuza kazi mkuu wa Polisi wa Shinyanga, Dar - es- salaam na unguja kama hawawezi kuhakikishia wananchi usalama wao. Onyesha kuwa uko madarakani (in charge) na sio kutapatapa kwa kuunda wizara mpya zisizo na kichwa wala miguu.

Suala ambalo Mh. Kikwete ameshindwa kung'amua mapema na huenda likasababisha akawa rais mvurugaji badala ya mjengaji ni hili hapa: Serikali kubwa huendeshwa na watu wengi ambao sio malaika. Maana yake ni wamba: kila binadamu kwa hulka zake huadawa na tamaa, ubwenyenye, kutojali na unyang'au . Point ni kwamba: Kuundwa kwa wizara mpya ya Usalama wa raia kunaweza kusisaidie chochote kile katika jitihada za kupambana na wimbi kubwa la ujambaza linalokabili Taifa letu kila kunapokucha endapo kama wale waliopewa dhamana ya kuongoza wizara hiyo (ambao sio malaika bali wanadamu) watahadawa na tamaa, ubwenyenye na kuishia kuwa watu wasiowajali wale walio wanyonge kuliko wao wenyewe. Kilichotakiwa hapa ni kuhakikisha kuwa watu wanawajibika ipasavyo na sio kuunda wizara mpya. Oya JK..!!!!!

Kinachosikitisha zaidi ni kwamba: wakati mataifa makubwa yaliyo na uwezo wa ku-balance na Kusimami bajeti zao wenyewe wanakuna vichwa na kuhangaika bila kulala ili kutafuta njia ya kupunguza ukubwa wa serikali zao hivyo matumizi, serikali masikini ya Tanzania isiyo na ubavu wa kusimamia bajeti yake walau hata kwa mwaka mmoja tu--yenyewe inajisifia na kujigamba kwa ukubwa wa serikali yake. Upuuzi mtupu!

Na sio suala la ukubwa wa serikali tu, [hapana!]. Ajabu ni kwamba, wakati dunia ya leo inasonga mbele kwa kasi ya aina yake kwa kuwatumia wataalamu vijana wenye fikira mpya na nyepesi--Kikwete yeye anaturudisha kulekule tulikokuwa miaka ya sitini kwa kutupatia vikongwe kama mzee Ngombale! Hivi Tanzania haina watu wengine wenye uwezo na hekima ya kuongoza zaidi ya mzee Ngombale Mwiru? JK unacheza...

Isitoshe, kwa dharau kabisa kikongwe huyo anapatiwa Wizara isiyoendana kabisa na falsafa zake! [O, great!] Kingunge anajulikana kuwa ni Msoshalisti hadi kufa kwakwe, utampatiaje yeye?

C'mon Kikwete, hii ndio kasi mpya uliyotuahidi wakati wa Kampeni ama unatutania..! Watanzania hususani vijana tunamategemo makubwa sana na serikali ya awamu ya nne [tafadhali, usituangushe]. Sote tu wadau kamili wa Taifa hili, acha kuchemka mapema kiasi hiki.

TUMA MAONI YAKO [HAPA]

Kwakweli hii ni dharau kabisa! Kingunge sio malaika--Tito

<<BACK TO MAIN PAGE >>

©Copyright:BongoTz.Com -MMV. All Rights Reserved.