TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA, NINI KIFANYIKE?

Na, Mathias Jackson

Wahenga walisema palipo na Miti hapana wajenzi,ni vigumu kujua mtunzi wa methali hiyo alikuwa na maana gani lakini walimu wangi wa Kiswahili hufundisha kwamba maana ya hiyo Methali ni kwamba palipo na mali hakuna watu wa kuweza kuitumia (utilize), na ukiangalia katika Dunia ya sasa ni kitu ambacho kikowazi kwa sababu ukiangalia mataifa mengi yaliyoendelea sio kwamba yote yana mali asili za kutosha mfano Norway,Marekani na nchi nyingine nyingi za Magharibi zilizoendela.

Tanzania ni kati ya nchi chache Duniani zilizojaliwa na mali asili za kutosha na kila aina. Mfano Ardhi yenye rutuba, Hali nzuri ya hewa,Mito na Maziwa yenye Samaki, Wanyama Pori na Milima ya aina mbali mbali ambavyo hivyo vyote ni vivutio vya Watalii ambavyo kama vingetumika vema Taifa lingejipatia pato la kutosha kuendeleza shughuli za kiserikali pamoja na jamii kwa ujumla, lakini kwetu sisi ni tofauti, tuna matatizo mengi hata zaidi ya Nchi ambazo hawana kitu chochote, na tatizo kubwa linalolikabiri Taifa kwa sasa ni ajira kwa vijana.

Kwa mtazamo wa haraka haraka tunaweza kugawa sababu zinaazosababisha ukosefu wa ajira kwa vijana Tanzania katika makundii mawili.Kundi la kwanza ni zile sababu zote zinazosababishwa na serikali kutokana na sera zake butu juu ya swala hili.Na sababu nyingine ni zile zinazozosababishwa moja kwa moja na jamii ya Watanzania wenyewe.

Katika kundi la kwanza mfano mzuri ni mfumo wa elimu. Elimu ya Tanzania ina mapungufu ya kutosha, hii ni kwa sababu kijana anapomaliza elimu ya sekondari ambayo ni ya msingi kabisa, huwa hana ujuzi wowote wa kazi Wa-spanish husema,aina hiyo ya elimu (la educacion` en Tanzania es muy teorica), kwa sababu sio wote anaopata nafasi ya kuendelea na elimu ya juu, hii inasababisha kundi kubwa la vijana kurundikana mitaani,na kuleta athari zingine kama ubakaji, uporaji, madawa ya kulevya.

Sababu nyingine ni rushwa,sio watu wote wenye uwezo wa kununua kazi, wakati mwingine mazingira yanatatanisha mno.Mathalani, utakuta kijana ana vigezo vyote vya kazi, ila kwa vile hana uwezo wa kutoa kitu kidogo,na kwa bahati mbaya masikini huyu hamjui mtu ( pale anapo omba ajira) basi hana zake tena, na kama tujuavyo sote kuwa rushwa ni adui wa haki kwa hiyo anakuwa amepoteza haki yake ya msingi na kuletea taifa matatizo makubwa kama vile kujihusisha na vitendo viovu. Ujambazi kwa mfano.

Zaidi ya hapo kuna tatizo la kutowapatia msaada (support) vijana hasa wanapo anziasha vikindu vidogo-vidogo kwa ajili ya kujiajiri wenyewe. Oh, wataanza kufuatiliwa juu ya ushuru ambao sio halari bali ulio kwa ajiri ya masilahi ya wachache tu--wakati kuna mashirika na viwanda vikubwa ambavyo hawalipi ushuru na zaidi ya hapo viwango wanavyo wawekea hao vijana ni zaidi ya uwezo wao. Itakumbukwa kuwa, Baba wa taifa katika moja ya hotuba zake alisema kwamba serikali yetu ya sasa haikusanyi mapato kama inavyotakiwa inakaa tu kukimbizana na wafanyabiashara wadogo wadogo ambao hawana lolote. Alikuwa anaisema serikali ya awamu ya pili kitu ambacho kipo hata leo hii.

Tatizo jingine liko kwa waajiri. Wao wanavutiwa saaaana na wazee kwa sababu wana walipa kiasi ambacho kinawasababisha wapate faida ya kutosha wakijua ya kwamba kuajiri vijana ni migogoro, kwa sababu watadai haki za msingi.

Sio hayo tu pia vijana nao wana matatizo yao yasiyoelezeka kwa urahisi. Mfano, vijana walio wengi wanachagua kazi hata sizolingana na ujuzi walio nao. Unakuta kijan hana ujuzi wowote na analaumu kwamba serikali haifai, bila ya kujali ujuzi wake. Katika moja yaa hotuba zake, Mheshimiwa Mkapa aliwahi kusema: Watanzania wasingoje serikali ifanye kila kitu, wanalo jukumu la kujiletea maendeleo wenyewe..., na zaidi ya hapo, tukirudi nyuma serikali ni nani kama sio sisi wenyewe.

Jambo la kushangaza ni kwamba serikali imeshindwa kuanzisha vyanzo vya kazi kwa vijana,Tanzania tuna ardhi kubwa ya kutosha na yenye rutuba jambo la msingi ni kuanzisha Plantation and Agro-base Industries.Kwani viwanda vingapi tunaweeza kuanzisha kwa mazao tunayo zaliisha na kuuza kwa Nchi jirani kama Kenya? Au ni ajira ngapi tunaweza kutengeneza kama tunaweza kuanzisha viwanda kama hivyo, lakini serikali haioni hilo zaidi ya hapo ina-imports kila kitu na hii inaleta ushindani na uuwaji wa hata vile viwanda ambavyo vilikuwepo na kuongeza watu wasiokuwa na kazi. Pia unakuta serikali ina-export primary products na hizi ni kutoa ajira kwa hizo nchi ambazo zina nunua mali ghafi kutoka tanzania.

Zaidi ya hapo Tanzania hatuna sheria ya kazi na kama ipo haifatwi.Utakuta mtu ana miaka 70 bado yuko kazini, na wakati kuna kijana mwenye miaka 23 au 28 hana kazi na wana ujuzi sawa. Mfano mzuri ni juu ya uteuzi wa Balaza la Mawaziri lililofanyika hivi karibuni, kwangu binfsi sielewi juu ya uteuzi wa huyu Mheshimiwa saaaaaaaaana Kingunge Gombare Mwiru, kwa sababu wako vijana wa kutosha na wenye akili inayochemka na wenye uwezo mkuwa wa kufanya kazi ila sisi kama watanzania utakuta jambo kama hili hatulioni, na zaidi ya hapo utakuta vyombo vya habari vinasifia kwamba Rais amewakumbuka wakongwe, je kwanini wasiulize juu ya Rais kuwakumbuka vijana?

Hiyo haitoshi kuna mambo mengine tukifikiria au ukimuuliza raia wa Nchi yeyote yule hatapata jibu cha zaidi atabaki kucheka. Hivi ni nini kitambulisho chetu sisi Watanzania? Kwa sababu hatuna vitambullisho vya uraia, na kupata pasipoti Tanzania ni Kitendawili, mimi kama Mtanzania ni haki yangu ya msingi kupata pasipoti kama kitambulisho au Kipande kama waitavyo wenzetu wa Kenya.

Jiulize ni watu wangapi (wageni-foreigners) wanaishi na kufanya kazi kinyume na sheria nchini Tanzania hasa katika maeneo ya mipakani? Nenda Tabora na Kigoma utaona jinsi Wanyarwanda walivyojazana, nenda Namanga Wakenya na Wasomali walivyojazana. Baya zaidi ni kwamba; hao wote wana ajira na kama sio Serikalini basi katika Mashirika binafsi, au wanatumia Mali Asili za Tanzania kujiajiri wenyewe kitu kinachopelekea kupunguza nafasi za ajira kwa watanzania. Sio nia ya maada hii kupinga wageni kufanya kazi nchini-la hasha!, ila kwanza watanzania wapewe kipaumbele,na kama watanzania wakizikataa hizo kazi basi wageni waruhusiwe kuzifanya.

Hatuwezi kumalliza hii maada bila kuangalia mchango wa Taasisi za Fedha katika ajira, ajira sio lazima iwe ya serikali au kutoka katika Kampuni binafsi, unaweeza kujiajiri, lakini turudi katika nchi yetu, Kuna Mabenki lukuki yanatoa mikopo ila tatizo ni viwango vya Riba, viko juu sana, na ukizingatia sera ya riba ni kwamba ukiweka pesa benk riba inapungua kadri pesa inavyozidi kukua, na katika utoaji , riba iaongeezeka kadri mkopo unavyo pungua, sasa jiulize ni biashara gani ambayo ni productive kiasi kwamba hao vijana wanaweza kupata hiyo riba na bado kubakia na kiasi fulani kwa ajiri ya kuendeleza miradi yao.

Mwisho, ushauri wa bure kwa ndugu zangu Watanzania, kwamba kwa sasa tuko katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, na siyo hiyo tu pia SADC na huko tuko katika mapambano ya kiuchumi, kwa hiyo inabidi tuwe Wazalendo kwa bidhaa zetu. Maana yake ni kwamba, tununue bidhaa za kitanzania ili kuinua uchumi wa Tanzania, na kutoa ajira kwa vijana wetu ni dhahili kwamba kama sisi wenyewe tutashindwa kununua bidhaa zetu nani atakuwa radhi kuzinunua, Wazungu wanasema Charty starts from Home. Kwa sasa inakadiriwa kwamba East Africa ina idadi ya watu wapatao milioni 95, ikiwa Uganda ni Milioni 26, Kenya 34 na Tanzania ni 35, kwa hiyo kwa simple mathematics utaona kwamba tunaidadi kubwa ya watu ukilinga nisha na nchi zingine , na ni dhahiri kwamba soko letu ni kubwa, kwa hiyo tusije tukafanya makosa yaliyofanyika karibu miaka 40 iliyopita na EAC, kwani kuna baadhi ya nchi zina maendeleo zaidi yetu kutokana na matunda ya hiyo miaka 1967-1977..

Zaidi ya hapo tunaomba Serikali ijaribu kulinda masoko yetu na Viwanda vyetu vya ndani ili kupunguza Competition kwani ni dhahiri kwamba Tanzania tunazalisha mali bora zaidi ya nchi zengine ila tatizo ni kwmba tumepumbazwa na baadhi ya wajanja wachache wanaopata faida kutokana na uingizaji wa bidhaa hizo. Lakini ukweli unabaki pale pale kwamba mambo yako Bongo, na zaidi ya hapo tuko na Malighafi za kutosha, Hongera Bibie Meghji, kwa hatua uliyochukua wakati wa usafirishaji wa magogo nchi za nje. Ni mategemeo yangu na ya Watanzania wengine kwamba hao Mawaziri wanao husika na Wizara hizo wataanza na moto mkali, na kujitahidi kuendeleza Tifa katika misingi aliyoiacha Mzee Ben.

TUMA MAONI YAKO [HAPA]

 

<<BACK TO MAIN PAGE >>

©Copyright:BongoTz.Com -MMV. All Rights Reserved.