DADA ZETU ACHENI KUJICHUBUA

Tatizo kubwa linalowakabili dada zetu wa kibongo ni kasumba kuwa: "uzuri ni kujichubua".Tunashukuru kuwa Nancy Sumari ametuonyesha kuwa si hivyo ilivyo! Ametuonyesha kuwa unaweza kung'ara katika medani ya urembo hata kama wewe ni pepsi tu na wala hakuna haja kabisa ya kujichumbua kiasi ca kufikia hadhi ya "pepsi-mirinda".

Dada zetu wa kibongo acheni mambo ya kujifanya mnakwenda na wakati kumbe mmepitwa na wakati. Ni jambo la aibu tena la kushangaza sana pale mwanamke anapojichubua kwa kutumia vidonge au njia mbalimbali ya kumfanya abadilike rangi na kusahau au kumletea kiburi Muumba wake aliyemuumba katika umbo lililo bora zaidi kuliko hilo analolitafuta na kulihitaji.

Rangi nyeusi ni yetu, hiyo ndio asilia tambulisha yetu [identity yetu]. Dada zetu munajidharirisha na kupoteza utu wenu asilia ( japo naamini wengi hamjui hilo) pale mnapoamua kwa kiburi tu kuamua kutumia mkorogo ili mfanane na ngozi nyeupe. Hebu jiulizeni hili swali: "Mbona mademu wa kizungu ama waasia hawakurupuki na kuanza kujipaka mkaa ili wafanane na ngozi nyeusi?" Acheni ulimbukeni jamani !!

Katika mashindano ya hivi Karibuni ya kumtafuta mrembo wa Dunia (Miss world-2005) yaliyofanyika mjini Sanya-China, tumeshuhudia kuwa: bila hata ya kujichumbua bado unaweza kung'ara vizuri katika medani ya sanaa ya urembo hata kwa urembo wako wa asili tu...

Pongezi nyingi zimfikie mrembo Nancy Sumari kwa kuitoa Tanzania kimasomaso katika mashindano ya urembo ya dunia mwaka huu. Nancy alianza kwa kuvikwa taji la mrembo mwenye mvuto pichani yaani Miss Photogenic , taji la Miss Kinondoni na kisha Miss Tanzania na sasa ndiye Miss World Africa.

Ukimuangalia pichani, ngozi yake nyororo na nyeusi , ngozi ya asili isiyo fahamu mkorogo ni nini, inawaka na kuvutitia kutia jicho. Si ajabu hicho ni kigezo kikubwa kilichomfanya walau aogelee na kufika kwenye sita bora na kunyakua taji la "miss World Africa".

 

--->Kong'oli [hapa] kwa picha zaidi <---

 

<<Back to main page>>

©Copyright:BongoTz.Com -MMV. All Rights Reserved.