SEHEMU YA- I

Ni saa nane kamili mchana (2Pm): Shenene akiwa na mdogo wake wa kiume Kevin, pamoja na babake---mzee Stadimire anawasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Marseille "Aerop`ot de Marseille" ulioko kusini-mashariki mwa Ufaransa tayari kwa safari yake kuelekea nchini Tanzania kumsalimia mama yake kipenzi (Gloria) aishiye Oysterbay jijini Dar-es-salaam.

Ghafla, uwanja wa ndege unazingirwa na makachero wa kifaransa pamoja na askari wa kikosi maalum cha kutengua mabomu cha Ufaransa( French Bomb Squad-FBS) .

Oh, shit,! Kundi la magaidi la kichechenia lilikuwa limetega bomu ndani ya ndege 'Boeing 743-200' iliyokuwa ikielekea Dar -es-salaam, na kisha kuwapigia simu wana usalama wa ki-faransa kuwajulisha kuwa kulikuwa na bomu ndani ya ndege hiyo...

Huku wakikimbiza na muda, askari hao wa kikosi maalum cha kutengua mabomu wakaanza kuchakarika kufa na kupona ili kutengua bomu lile. Iliwachukua askari hao takribani masaa matatu hivi kufanikisha zoezi zima.

Baada ya kukurukakara hizo,mnamo majira ya saa kumi na moja u-nusu jioni,abiria wakaruhusiwa kuingia ndani ya ndege tayari kwa safari ya kuelekea Dar.

"Bon Voyage--safari njema sweet," Mzee Stadimire akampulizia binti yake busu kwenye shavu la kulia, kisha akamkumbatia na kumuuaga..., Kevin naye akafanya vivyo hivyo.

Punde pipa likaanza safari kuelekea Bongoland.Kwa muda wa masaa manane na nusu Boeing 743-200 ilikuwa angani ikiyakata mawingu kwa mwendo mtoroko wa sayari magrini...

Ilipotimu saa saba kaso-robo usiku;sauti ikasikika mle ndani ya ndege kwanza kwa kingereza kisha kiswahili; "Mabibi na mabwana fungeni mikanda...tunakaribia kutua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar-es-salaam.., natumaini mmekuwa na safari njema."

Kutokana na kitimutimu kilichotokea Mjini Marselle na kusababisha ndege aliyokuwemo Shenene kuchelewa kuondoka mapema na hatimaye kuchelewa kufika Dar katika muda uliokuwa umepangwa. Uncle Mangushi--mwenyeji wake aliyekuwa ampokee,alikata tamaa na kuamua kuondoka mapema kabla hata ndege haijawasili.

"Mbona simuoni uncle-Mangushi," Shenene alijiuliza huku akiangaza macho huku na kule... Mara akaona Toyota Mark II nyeupe imepaki pembeni nje ya rango la kuingilia airpot.Lakini alikuwa hajui ni nani aliyemo ndani ya gari lile. [Mhh!] Alikuwa ni "Kapteni"-kama wengi walivyomjua pale airport.Lakini Jina lake halisi aliitwa Twidi wa Mvevidi.

Shenene akasogelea ile Mark-II na kusema,"Oh,samahani kaka,nilidhani ni gari ya uncle Mangushi...," akapozi kidogo kisha akaendelea, "alitakiwa kunipokea leo saa nne usiku,lakini ndege yetu ilichelewa kuondoka Marselle-Ufaransa na kutufanya tuchelewa kufika."

"No, bila samahani sister," Kapteni akajibu na kuhoji, "Kwani unaelekea wapi?"

"Oysterbay, kwa mzee Stadimire." Shenene akajibu.

"Una maanisha ile nyumba nyeupe yenye vigae vyekundu, iliyopo nyuma kidogo ya 'Oysterbay Shopping Centre'. ..," Kapteni akadakizia.

"Ha, ha, ha...," Shenene akacheka na kuitikia "...ndiyo,umepajuwaje wewe?"

"Mimi mwenyeji mitaa ile,bosi wangu anakaa nyumba ya tatu toka unapokaa...,mimi mwenyewe naelekea hukohuko..." Kapteni akachomekea na kumwambia Shenene aingize mizigo ndani ya gari.

Basi,wakaanza mwendo kuelekea Oysterbay.Wakiwa njiani--Sheneni akauliza,"itagharimu kiasi gani kaka?," "Shilingi elfu tatu." Akajibu Kapteni.

"Hapa nilipo nina franc tu, sina chenji za kitanzania. Naomba uniachie namba yako ya simu kisha kesho asubuhi nikisha badili nikutafute..." Shenene akasihi.

"No, usikonde. Mwenyewe naelekea hukohuko kwahiyo usijari," Kapteni akamtuliza.

Muda si Muda wakafika Oysterbay.Shenene akashusha mizigo na kumshukuru brother Kapteni kwa usamalia wake kisha akamuaga na kuingia ndani.

Kesho yake asubuhi Kapteni akasikia kilongalonga chake kinaita :"Hallo.., ni mimi Shenene...nilikuwa nahitaji kukupa 'special thanks' Kwa msaada ulionipatia jana usiku, sijui kama utakuwa na nafasi leo jioni..."

"Ah, jioni ya leo..., saa ngapi vile na mahali gani?" Kapteni akauliza.

"Well,unaonaje tukikutana Golden Tulip leo saa tatu usiku,"-Shenene akarudishia.

"poa--haisumbui sister," Kapteni akatia mapozi.

Jioni ile Shenene akavalia kivazi chake kifupi na kizuri kilichokuwa kinaonyesha uzuri wa umbile lake lisilo na kasoro. [Asikwambie mtu jibaba!] Shenene alikuwa sister aliyeumbika haswa! Fiqure ya nguvu,ngozi nyororo ,na huko nyuma...mtumeee!,sister alikuwa kajazia kwelikweli. ..

 

SEHEMU YA -II

Golden Tulip Hotel: Ni saa tatu dk ishirini na tano usiku.Motokari moja ya nguvu yenye rangi ya kijani inawasili kwenye viunga vya Hotel Tulip.Kila mtu anachungulia kwa nje kuona ni nani atakayeshuka toka ndani ya poropilo ile.

Ile Rav4 ikapaki pembeni mwa Hotel.Watu wakazidi kunyenyua vichwa vyao juu kwa shauku ya kutaka kujua ni kimwana gani mwenye ile motokari nzuri.

Ghafla, ikachomoza miguu mizuri yenye umbo la chupa ya bia. Na wakati akishuka chini, kivazi kifupi alichokuwa amevaa kikaachana kidogo na kuonyesha sehemu ya juu ya mapaja laini yaliyokuwa yamesheni vema na kushindiliwa vilivyo..[damn!!].Hawajakaa sawa,akashuka binti mmoja wa nguvu aliyekuwa amevalia kivazi cha rangi ya purple chenye michirizi ya zambarajadi mabegani. [Mhhh!!] Alikuwa ni mtoto Shenene aishiye mjini Marselle,Ufaransa aliyekuwa jijini kumsabahi mama yake kipenzi.

Asikwambie mtu jibaba! Mtoto alikuwa kaiva! Ngozi nyororo isiyo na vipele wala chunusi ilikuwa inawakawaka...,huko nyuma nako "mambo ilikuwepo!!!!!"

Basi, alipokuwa anapiga hatua mbili-tatu kuelekea ndani, akasikia mtu akimgusa begani.Taratibu akageuka kwa pozi kali kumtizama huyo anayemgusa ni nani...,[Oh!] alikuwa ni Kapteni-kijana wa Mvevidi..

Shenene akamsogelea kwa karibu na kumpatia hug la nguvu na kisha kumpulizia kisa la shavu..

"Hi, Shenene,unaendeleaje?," Kapteni akawahi kutoa salamu.

"Salama sijui wewe..." Shenene akaitikia.

"Inshalah!, yote mema..." Kapteni akaitikia huku akitoa tabasamu la kuambikiza.

Baada ya kujuliana hali,wote wawili wakashikana mikono na kuelekea ndani...Wakiwa floor ya kwanza [sanaa restaurant],akapita mhudumu na kuuliza ," Masai Bar ama...?"

"Shenene akajibu, yes please...!"

Basi mhudumu yule akawapeleka na kuwaonyesha 'The Masai Bar' ilipo. Mle ndani wakaanza kukata mvinyo. Haikumchukua muda Shenene kabla macho hayajaanza kumlegea.

"Kapteni,nataka ufanye mapenzi na mimi hapa hapa...," Shenene alisikika huku akimsogelea.

Lakini kapteni hakuwa tayari kuyapeleka mambo haraka."No, haiwezekani Shenene..., tumekutana jana tu wala hatujuani vilivyo,leo unataka tufanye mapenzi tena hapa hapa?" Kapteni Akahoji.

Shenene alikuwa haambiliki kabisa, maana si yeye ila pombe ndani yake ndiyo ilikuwa inazungumza.

"Kapteni, I love you. Kuna kikubwa zaidi ya hicho?" Shenene alihoji huku akizidi kumsongelea Kapteni kwa karibu...

KUSOMA SHEMU INAYOFUATA: [Kongoli hapa>>]

 

©Copyright:BongoTz.Com -MMV. All Rights Reserved.